UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Wednesday, December 5, 2012

SHUKRANI ZA DHATI KWA WANACHAMA WOTE

habari zenu wanachama,

Kwanza kabisa kipekee kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa wema wake wote na uaminifu wake kwangu, kwa kuniongoza vema hadi siku ya leo.

Pili napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wanachama wenzangu kwa kuniamini na kunipa mamlaka ya kuongoza chama chetu kwa vipindi viwili mfululizo, kwangu ni heshima kubwa nimepewa na hakika sikuwaangusha, tumeanza chama tukiwa watu sita na shilingi sifuri hadi leo tuko wanachama zaidi ya hamsini, ni mafanikio makubwa sana na hili ni jambo la kushukuru,

Vile vile nawapongeza sana kwa uvumilivu wenu mlioonesha kwa kipindi hiki chote kwani mmekuwa pamoja nasi, tulikinzana sana kwa hoja nyingi lakini demokrasia siku zote ilitumika na maamuzi mengi yalitolewa kwa mujibu wa katiba inavyotuagiza tufanye, hili liko wazi na wanachama nyie ndo mashahidi wa hili, nimeisimamia katiba kikamilifu, tumetengeneza misingi mizuri ya chama, tumekuwa na ushirikiano wa karibu sana, umoja umejengeka, matukio mengi yaliyotokea katika kipindi chote hiki tumeweza kuyakabili kwa umoja wetu na mshikamano, na hii ndo alama sahihi ya ushiriki wenu mzuri katika uwezeshaji wa mipango ya chama kutimia kwa mujibu wa mipango sera na taratibu za chama tulizojiwekea.

Umoja wenye watu wengi kiasi hiki, lazima una mambo mengi sana yenye kukinzana sana lakini ni lazima tutumie vifungu vya sheria zetu ndogondogo tukitanguliwa na katiba, huku busara ikitawala katika kufanya maamuzi, tumelifanya hili bila kutetereka, na kwa manufaa ya chama chetu, nawashukuru sana,

Lakini ni lazima tutambue kuwa, tunayo safari ndefu sana, tulipofika sio pabaya, ni wakati sasa wa kuendeleza nguvu yetu ya ujana, akili zetu na nia yetu kuleta mawazo na fikira zenye upeo wa kujenga na kuimarisha umoja wetu ili malengo ya muda mrefu na mfupi yatimie, Kiongozi sio cheo ni kuonesha njia, hivo anahitaji sana uwepo wenu na michnago yenu ili afanye majukumu yake kwa ufasaha, tumewachagua viongozi wetu wapya sita pamoja na kamati ndogondogo kwa mujibu wa katiba, ninachoomba, juhudi mlizionesha na uungaji mkono wa yale yote tuliyofanya, naomba sana nguvu zetu tuzielekezee kwa UONGOZI MPYA, ninayo imani na hakika watu tuliowachagua hawatatuangusha, tunahitaji sana kuvumiliana, tunahitaji sana kuendeleza misingi ya kuheshimiana na kijaliana, naamini Mungu yu pamoja nasi.

Asanteni sana
Japhet