UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

HISTORIA FUPI YA CHAMA NA MALENGO YETU

Hiki ni chama cha umoja wa vijana wa Kata ya Kanyigo Mkoani Kagera, ambao wameamua kuunganisha nguvu zao ili kukabili changamoto zinazowakumba iwe kwenye furaha au majonzi, ni chama ambacho kilianzishwa mnamo 10.10.2010 kikiwa na wanachama 14 tu, kikiwa na malengo makuu manne ambayo ni
1.    i) Kuwa chombo cha kusaidia wanachama au mwanachama katika shida
       na raha
ii) Kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kuhakikisha kikundi kina uwezo wa kutekeleza shughuli zake.
iii) Kuwa na mawasiliano ya karibu na kuishi kama ndugu
iv) Kusaidia/kushiriki katika shughuli za kijamii
     
Zaidi tumelenga pia kusaidia kwa njia yoyote ili kata yetu ya Kanyigo iwe kwa ushauri, michango ya aina yoyote na nyanja zingine kulingana na uwezo wetu utakavyokuwa umeimarika.

Ikumbukwe maendeleo hayawezi kuletwa na mtu mmoja, ni lazima tushirikiane kukamilisha nia na dhamira ya watangulizi wetu pamoja na mawazo na ndoto zetu pia, tunatoa wito kwa vijana wote wa Kanyigo, mtuunge mkono ili baadae tuione Kanyigo tuitakayo. 

Ikumbukwe pia Chama hiki si cha kibiashara bali kimeundwa kwa nia ya kusaidiana kwa namna mbalimbali juu ya changamoto zinazotukabili sisi kama vijana.
Tunawakaribisha wale wote wenye mapenzi mema ya Kata yetu ambayo maendeleo yake hayaridhisha iwe kielimu, kiuchumi na hata maendeleo mengine kwa ujumla wake.

Imetolewa na Japhet Mukala
Mwenyeki wa chama



No comments: