UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Monday, July 22, 2013

TAFAKAKURI YA KINA NA Japhet Mukala.

Habari wanajamvi,

Ni jambo la kheri sana kuona watu wa jamii flani wanaamua  kuishi, kula pamoja, kunywa, kusaidiana kwa pamoja, kuteta, kujenga na kufanya mambo kadha wa kadha kwa mujibu wa makubaliano yao wenyewe waliojiwekea,
 
 Kutokana na changamoto nyingi sana za maisha ndo huwa chachu ya kusuku watu wawaze na kuunda chombo au jumuiya, au umoja au chama chenye lengo la kukabiliana na changamoto hizo nia hasa ya umoja ni kuunganisha nguvu ya wengi, mawazo na ushauri ili kufikia malengo husika.
 
Haya ndo mawazo na maswali mengi sana juu ya maisha na changamoto nyingi sana ndo vilitusukuma tuwe na mawazo ya kuwa na jumuiya ya vijana wa Kanyigo wanaoishi Dar es slaam. Halikuwa suala rahisi lakini kwa msaada mkubwa wa wanachama waliona agenda ina maana sana katika maisha yetu, waliikubali na kuipitisha hadi leo tumekuwa na chama cha vijana wa Kanyigo wanaoishi Dar es salaam Tanzania na nia ya baadae ikiwa ni kuunganisha vijana wa Kagera kwa lengo la kuwa na sauti moja juu ya agenda zinazohusu vijana na maslahi ya Mkoa wetu kwa ujumla.
 
Ebu jiulize kidogo maswali machache alafu tafakari majibu yake.
 
1.68% ya maprofesa hapa Tanzania wanatoka Kagera, je wana mchango gani katika Mkoa?
2.Ukilinganisha elimu ya Mkoa wa Kagera tangu miaka ya 90 hadi leo kuna tofauti kubwa sana, elimu imeshuka sana, je Tatizo ni nini?
3. Zao kuu la mkoa wa Kagera lilikuwa Kahawa na ndizi, walio wengi sana miongoni mwetu Kahawa zimetusomesha, lakini ukiangalia mwennedo wa zao hili umekuwa wa kusuasua, je kushuka kwa hili zao, je wana wa Kagera wanategemea zao gani hali hata ndizi zimeshambuliwa na magonjwa mengi sana?uchumi wa kagera unategemea nini?maisha ya walio wengi wanayaendeshaje?
 
Haya ni baadhi ya maswali yanahitaji majibu ya kina, ni mimi na wewe runaotakiwa kuja na majibu ya maswali haya.
 
TUJIPANGE.