UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Monday, January 14, 2013

GET TOGETHER EVENT 23.02.2013

Habari wanachama,

Rejea kikao kilichopita, tumekubaliana siku ya 23.02.2013 tutafanya get together party ya mwaka wa jana, ikumbukwe, tulishindwa kufanya hii party ambayo ipo kwa mujibu wa katiba kutokana na mambo kuwa mengi ndani ya kalendar ya chama, kuna mengi sana yatafanyika siku hiyo, msikose kwani ni kosa kikatiba kukosa siku hiyo. Mahali tulikubaliana siku ya kikao inagawa mtatumiwa tena sms kukumbushiwa na mipango mingine ya chama kuhusu siku hiyo.

Imetolewa na japhet Mukala

Wednesday, January 2, 2013

SALAM ZA MWAKA MPYA 2013

Ndugu wanachama,

chama cha vijana wa Kanyigo wanaoishi Dar es salaam, kinapenda kuwapongeza wanachama wote kwa kufanikiwa kumaliza mwaka 2012 kwa usalama na kuingia mwaka 2013, hii ina maana kubwa sana kwetu, ni mengi yametokea ndani ya 2012, lakini Mungu ametusimamia na tumevuka kwa usalama, tujifunge mkanda ili kukabili changamoto zilizo mbele yetu! nina imani tutashinda katika yeye atutiaye nguvu.

Muwe na baraka njema katika shughuli zenu za kila siku
Mungu abariki kazi ya mikono yenu na zaidi msisahau kufanya kazi kwa bidii na malengo
Mwisho, tukumbuke ibada.
Japhet Mukala.