UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Sunday, October 16, 2016

Salam za jumapili

Patrick Kalungu Banda,  rafiki yangu mzambia aliyeishi Tanzania miaka 7 aliwahi kuniambia maneno ambayo hadi leo nayakumbuka,  alisema binadamu ni viumbe wa ajabu sana,  wapo wanafiki,  wambea,  wasema hovyo, akasema wapo pia ambao midomo yao huwa inawasha wasipofungua midomo na kusema chochote,

Wapo pia wenye Upendo, wenye kuombea wenzao mema,  wenye huruma na hofu ya Mungu, Aliniambia Kamwe usishughulike na kundi ambalo halitakupa faida,  kundi ambalo linataka udodondoke,  ufilisike,  uugue,  unapofail kwa kila jambo ndo Furaha yao,  Aliniambia kuwa Hawa ni sawa kabisa na wachawi,  akanishauri nitumie Muda mwingi kudeal na mambo yatakayonipa faida,  yatakayinijenga kiroho na kiakili,  yatakayoniongezea marafiki wa kweli, yatakayonipanulia wigo Wa kibiashara n. k. shetani halali kamwe lakini pamoja na yote usimruhusu akusogelee, badala yake  aendelee kukuona unasonga mbele tena kwa speed kubwa. Muwe na jumapili njema watu Wa Mungu

No comments: