UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Wednesday, November 23, 2011

NUKUU YA LEO

WOGA NI ADUI WA HAKI, TUSIMAME IMARA KUKEMEA NA KUTETEA HAKI ZETU

Wednesday, November 9, 2011

MATENDO, JUHUDI NA JITIHADA ZETU NDO ALAMA SAHIHI YA UJANA WETU

Sisi kama vijana tunayo nafasi kubwa katika jamii kuhakikisha mambo yanaenda, sisi ndo nguvu kazi na sisi ndo daraja sahihi kati ya wazee wetu na wadogo zetu, tunao wakati mgumu sana kuhakikisha gurudumu linasogea kwa kadiri inavyotakiwa.

wazo la kuwa na chama lilikuwa lazima liwepo hii ikiwa ni sababu ya kuuunganisha nguvu zetu juu ya jambo fulani tulililo amua kulifanya, lazima tuwe na common agenda na hii ajenda lazima ishirikishe watu wenye kariba mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine watashirikiana katika kuhakikisha hili jambo linafanyika kwa ufanisi mkubwa.

Sisi kama vijana lazima tuoneshe mfano mzuri katika jamii ambao hata wadogo zetu utawapa mwanga bora wa maisha na vilevile iwapo tutaamua kwa sauti moja kukamilisha yake tuliyoyapanga nina imani itajenga imani sana kwetu na tutakuwa tumejiwekea heshima kubwa sana juu ya uso wa dunia.

TUNAKARIBISHA MAWAZO YENU ILI TUJENGE CHAMA

Sisi kama chama, nia na madhumini hasa ni kuhakikisha malengo ya chama kama yalivyoainishwa kikatiba yanatimia, sisi kama sisi hatuwezi bila michango ya mbalimbali ya wadau!njoo ujiunge na sisi, njoo ujifunze na sisi kwani naamini mikusanyiko yetu ni moja ya madarasa ya kijamii! tunapatikana kwa http://www.vijanakanyigo.blogspot.com/ au facebook .ni. vijana kanyigo na email yetu ni vijanakanyigo2011@yahoo.com .tunawakaribisha sana na tunakaribisha mawazo yenu.
by japhet mukala-mwenyekiti wa chama.

MIKUTANO YA CHAMA KIKATIBA


MIKUTANO YA CHAMA KIKATIBA

                10. Chama kitakuwa kinafanya mikutano ya aina tatu (3) kama ifuatavyo.

10.1.Mikutano ya kila jumapili ya mwanzo wa mwezi ambayo itakuwa imelenga zaidi kuwa na mawasiliano ya karibu kati ya mwanachama na mwanachama na kuangalia lipi lifanyike ndani ya chama ili kuleta ustawi imara na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha chama

10.2 Mikutano ya kila robo ya mwaka itakayopitia mwenendo wa chama kwa kila robo mwaka na kufanya marekebisho ipasavyo au kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kutoka kwa wanachama.

10.3. Mkutano wa dhararu ambao utawahusisha wanachama wote au kamati ya uongozi pindi itakapobidi kuwa hivo na hii itatokana na jambo ambalo litakuwa mbele yetu na kudhibitishwa na mwenyekiti wa chama.

Mahali pa kukutana ni TP MAZEMBE, iko nyuma ya ubungo plaza karibu sana na uwanja wa mpira, na muda ni saa tisa na nusu hadi kumi na mbili na nusu. mwanachama mwenye ajenda binafsi ili ijadiliwe na wanachama inatakiwa uwasilishwe kwa katibu mapema ili uongozi upate muda wa kuiangali umuhim wake na kuitolea ufafanuzi...

Mgeni aliye alikwa hatakuwa na fursa ya kujadili hoja au ajenda iliyoletwa mezani hadi pale atakaposajiliwa kama mwanachama kamili ingawa anaweza kupewa nafasi ya kushauri.