UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Wednesday, November 9, 2011

MIKUTANO YA CHAMA KIKATIBA


MIKUTANO YA CHAMA KIKATIBA

                10. Chama kitakuwa kinafanya mikutano ya aina tatu (3) kama ifuatavyo.

10.1.Mikutano ya kila jumapili ya mwanzo wa mwezi ambayo itakuwa imelenga zaidi kuwa na mawasiliano ya karibu kati ya mwanachama na mwanachama na kuangalia lipi lifanyike ndani ya chama ili kuleta ustawi imara na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha chama

10.2 Mikutano ya kila robo ya mwaka itakayopitia mwenendo wa chama kwa kila robo mwaka na kufanya marekebisho ipasavyo au kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kutoka kwa wanachama.

10.3. Mkutano wa dhararu ambao utawahusisha wanachama wote au kamati ya uongozi pindi itakapobidi kuwa hivo na hii itatokana na jambo ambalo litakuwa mbele yetu na kudhibitishwa na mwenyekiti wa chama.

Mahali pa kukutana ni TP MAZEMBE, iko nyuma ya ubungo plaza karibu sana na uwanja wa mpira, na muda ni saa tisa na nusu hadi kumi na mbili na nusu. mwanachama mwenye ajenda binafsi ili ijadiliwe na wanachama inatakiwa uwasilishwe kwa katibu mapema ili uongozi upate muda wa kuiangali umuhim wake na kuitolea ufafanuzi...

Mgeni aliye alikwa hatakuwa na fursa ya kujadili hoja au ajenda iliyoletwa mezani hadi pale atakaposajiliwa kama mwanachama kamili ingawa anaweza kupewa nafasi ya kushauri.



No comments: