UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Monday, December 19, 2011

WAKATI TUNAJIANDAA KUSHEREHEKEA SIKU KUU YA XMAS



Ndugu wanachama,

Namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufika hapa leo tukiwa wazima wa afya, ni rehema yake tu kuona hadi leo tunavuta pumzi yake,inabidi tumshukuru sana na kumtukuza  Mwenyezi kwa kutenda yaliyo mema kila wakati.

Kwa niaba ya chama cha vijana wa kanyigo, napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza na kuwatakia sikuu njema yenye furaha na matumaini katika maadhimisho ya kuzaliwa kwake yesu kristo, ni furaha sana na ni siku muhimu ya kutafakari matendo yetu, kujiuliza sababu hasa ya kuzaliwa kwake yesu, kama ilikuwa kwa ajili ya dhambi zetu je tunayatekeleza yale aliyotwambia kuyafuata yale aliyotuachia kama urithi sahihi wa kuuona ufalme wa mbingu, tujiulize ndani ya kipindi chake cha kuhudumu cha miaka mitatu je alitimiza yale yote aliyokusudia kufanya hapa duniani duniani?kama sio yote ni nani anatakiwa kuyakamilisha yale yaliyokusudia na ni kwa jinsi gani tunaweza kuyakamilisha na kwa msaada wa nani? ni nini alitwambia kufanya juu wa ufalme wa mbingu?

Nadhani ni maswali magumu sana, inahitaji muda mwanana, busara na wigo mpana katika kutafakari majibu yake wakati huu wa maadhimisho na baada ya maadhimisho, tusherehekee kwa taadhari na tafakari yenye tafakuri timilifu, na upembuzi yakinifu juu ya matendo na matakwa yampasayo mwanadamu kuyafata ili awe mkiristu aliye na haki mbele za mungu na kwa njisi gani mwanadamu anaweza kuwa na haki mbele yake aliye juu.

Mwisho niwatakie sherehe na baraka njema pamoja na familia zetu kwa ujumla
Tukumbuke kuwaombea walio kwenye mateso mbalimbali, walio wagonjwa, walio na njaa, waliohukumiwa, waliokosa matumaini, waliosafarini, hata wasioamini juu ya wokovu wa mungu., waliombali na familia zao, walio vitani, wanaopambana na uovu kila kukicha. Mungu ni mwema siku zote!

imani zetu ziwe ndani ya utatu mtakatifu yani, ''mungu baba, mungu mwana na roho mtakatifu'' amina
Imetolewa leo 19122011  na
Japhet Mukala

WISH U A MERRY XMASS

 

Thursday, December 15, 2011

SALAMU ZA PONGEZI KWA WANACHAMA WETU

Kwa niaba ya chama cha vijana, napenda kuchua fursa hii kuwapongeza wanachama wenzetu
1.Tunampongeza Denis Rutahilwa kwa kujaliwa kupata mtoto
2.Abdul Kyaijunga kwa kujaliwa kupata mtoto
3.Tunampongeza Stanley Pesha kwa kumaliza chuo (Tanzania institute of Accountancy) na tunamtakia sherehe njema hapo kesho 17.12.2011

Chama tuko pamoja nao katika sherehe kubwa na mafanikio makubwa, hii ni hatua muhimu katika maisha
mungu awatangulie na kuwalinda watoto wote waliozaliwa na tunawakaribisha kwenye familia mpya ya vijana wakanyigo ambao ndo wanachama watarajiwa, pili tunampongeza sana Stanley na kumtakia mafanikio mema na kumkumbusha kulitumikia taifa kwa uadilifu mkubwa ili kujenga nchi yenye vijana imara na wenye uchungu na uchu wa maendeleo ya nchi yao.

imetolewa leo na 16122011
Japhet Mukala
mwenyekitu

MKUTANO WETU WA 16 MWEZI JANUARY 2012

Ndugu wanachama, rejea na kichwa cha habari hapo juu, kutokana na ukweli wa mambo ni kwamba, katiba inasema makutano yetu ni kila jumapili ya mwanzo wa mwezi, na mwezi january jumapili ya mwanzo wa mwezi ni tarehe 01.01.2012 ambayo kimsingi ni sikukuu ambayo watu wataitumia kukaa na kusherehekea mwanzo wa mwaka na ndugu pamoja na familia zao, kwa maana hiyo, kama tulivyokubaliana kikao cha tarehe 4 dec 2011, tutakutana jumapili itakayofuata ambayo ni tarehe 08.01.2012 saa tisa na nusu juu ya alama jioni, mnaombwa sana kukumbuka na kuzingatia muda pamoja na maazimio ya chama.

Imetolewa leo 15122011 na
Japhet Mukala
Mwenyekiti.

Wednesday, December 14, 2011

MAMBO YA KUKUSAIDIA UNAPOWEKA MALENGO YA MWAKA 2012

MAMBO YA KUKUSAIDIA UNAPOWEKA MALENGO YA MWAKA 2012
Katika kuumalizia mwaka huu wa 2011 nataka nikutafakarishe kwa kukuuliza swali hili, je malengo yako uliyojiwekea katika mwaka 2011 katika nyanja mbalimbali kama vile kiroho, kihuduma, kifamilia, kikazi, kibiashara, kiuchumi nk yamefanikiwa kwa kiwango gani? Na kama hujafanikiwa je umejiuliza kwa nini hujafanikiwa kwa kiwango ambacho unaamini ulitakiwa kufanikiwa? Je, umegundua nini ni vikwazo vya wewe kufikia malengo yako?
Kama ukiyatafakari maswali hayo hapo juu utagundua kwamba najaribu kutaka kujua kama kwanza huwa una tabia ya kuwa na malenngo, na kisha kuweka mikakati inayotekelezeka ili kufikia hayo malengo, na mwisho kufanya tathimini   mara kwa mara ili kupima malengo yako yanafanikiwa kwa kiwango gani kadri siku zinavyozidi kwenda.
Kuna tafsiri nyingi za malengo na hasa kwa kutegemeana na kile unachotaka kukipata au kukifikia, lakini tafsiri rahisi zaidi ni hii. Malengo ni hatua fulani katika maisha ya mtu ambayo hajaifikia na hivyo anataka kuifikia. Na jambo la msingi, unapaswa kufafanua vizuri lengo husika ambalo unataka kulifikia. Ufafanuzi mzuri wa lengo au malengo yako utakusaidia katika kujiwekea mikakati mizuri yenye kutekelezeka.  
Katika ujumbe huu mfupi wa  funga mwaka ya 2011 nataka tu kukumbusha mambo kadhaa ya msingi yatakayokusaidia unapoanza kuweka  malengo ya mwaka 2012.
Jambo la kwanza; Weka malengo yako mapema, kwa kuzingatia vipaumbele vyako.
Ni vema ukaweka malengo ya mwaka unaofuata kabla mwaka huo haujaingia. Mfano, kama mpaka sasa bado hujaweka malengo unayotaka kuyafikia katika mwaka 2012 basi tumia muda huu uliobaki kufanya kazi hiyo. Kwa nini nasema jambo hili, hii ni kwa sababu utekelezaji wa malengo yako unapaswa kuanza tarehe 01.01.2012 kama tukifika kwa neema yake Mungu.
Kwa hiyo kama tarehe hiyo ikifika hujapanga malengo yako jua kwamba tayari umeanza vibaya na kuna uwezekeano mkubwa wa kutokufikia malengo yako. Ikiwa ulishaweka malengo kwa kipindi cha mika mtatu, mtano au zaidi, bado pia unalazimika, kuyafafanua vizuri hayo malengo yako kwa kuzingatia mazingira yaliyopo na rasilimali utakazohitaji. Naam unapoweka malengo kumbuka kuyawekea  muda wa hilo lengo kufikiwa.
Kwa uzoefu wangu katika kuweka malengo kikazi,kihuduma,kiuchumi, kifamilia, nk, nimejifunza na kugundua kwamba malengo ni muda, malengo ni mikakati na kisha malengo ni nidhamu uliyonayo katika kutekeleza mikakati na hasa ile inayohusu fedha. Muda ni ufunguo mkubwa wa kukusaidia kufikia malengo yako. Ukicheza na muda, huwezi kufikia malengo yako. Na kwa sababu hii ni lazima ujifunze kufikiri kimuda na kim-kakati kwa kila lengo unaloliweka.  
Naam kufanikiwa kwa malengo ya Mtu binafsi, Shirika, Serikali nk kutategemea namna mtu/watendaji wa Serikali au Shirika husika wanavyotumia muda walionao, mikakati iliyopo na mwisho nidhamu yao katika utendaji wao.  Naam, mambo haya matatu yakizingatiwa yatafanyika funguo za kufikia malengo yako au ya Shirika lako.  
 Jambo la pili: Weka mikakati ya kutekeleza malengo yako 
Ili malengo yako yaweze kutekelezeka, sharti uwe na mikakati inayotekelezeka, vinginevyo huwezi kuyafikia malengo yako. Mikakati ni mbinu, njia utakazotumia katika kutekeleza malengo yako. Naam kwa kuwa malengo yako yanakuwa ndani ya muda fulani ni lazima na mikakati nayo iwe kimuda. Katika kuweka mikakati, kuna baadhi ya malengo yatakutaka ushirikiane na baadhi ya watu, sasa kuwa makini na nani unashirikana naye katika kuyafikia malengo yako.
Jambo la tatu: Fanya tathmini ya utekelezaji wako wa malengo
Watu wengi sana, huwa wanasahau sana hiki kipengele katika utekelezaji wa malengo yao, na ndio maana si wengi wanaofikia malengo yao. Tathmini unaweza ukafanya kwa vipindi viwili au vitatu kwa mwaka. Maana yangu ni kwamba unaweza uka-ugawa mwaka mara mbili na hivyo kuamua kwamba utakuwa ukifanya tathmini zako mwezi wa sita na kumi na mbili. Naam huu ndio mfumo ambao mimi binafsi huutumia. Hata hivyo kuna baadhi ya malengo huwa nayafanyia tathmini yake kila mwezi, ingawa tathmini kubwa huwa nafanya Juni na Desemba. Katika kufanya tahmini jambo kubwa ni kuangalia mikakati yako imekusaidia kwa kiwango gani kufikia malengo yako.   
Jambo la nne: Boresha malengo kadri muda unavyokwenda, kwa kuzingatia tathmini unayoifanya.
Kama katika tathmini unayofanya mara kwa mara umegundua kwamba kuna lengo au malengo haya tekelezeki, basi kwanza litazame hilo lengo tena vizuri, kisha mikakati yake. Lazima kama siyo lengo, basi mikakati unayotumia haijakaa vizuri, na kwa hiyo unaweza kuliboresha lengo lako vizuri na hvyo mikakati yake pia. Mimi hutumia tathmini ya mwezi wa sita kurekebisha baadhi ya malengo na kisha kuboresha mikakati yake. Na kisha baada ya tathmini kubwa ya Desemba ndipo pamoja na mke wangu tunaweka malengo yetu ya mwaka unaofuta. Jambo la msingi hapa ni kuhakikisha kwamba malengo tunayoweka kila mwaka yanalenga kutufikisha kwenye malengo yetu ya miaka mitano mbele, tuliyokwisha kuyaweka tangu mwanzo.
Jambo la tano: Jenga mazoea ya kuyasoma na kutafakari malengo yako mara kwa mara.
Jambo hili litakuwekea msukumo wa kuhakikisha unatekeleza mikakati yako ili kuyafikia malengo yako. Mfano unaweza kuweka malengo yako kwenye Laptop/Computer yako,  unaweza ukaweka malengo yako kwenye meza yako ya kusomea au unaweza ukaweka ‘Remainder” kwenye simu yako iwe inakukumbusha kila wiki kupitia malengo yako nk. Hata hivyo ni vema ukaweka, malengo/mikakati yako, mahali ambapo ni salama kwa maana ambayo haitakuwa rahisi kwa mtu au watu wengine kuona, Shetani asije akawatumia hao katika kukwamisha malengo yako.
Kutokana somo hili, hebu angalia katika mwaka wa 2011 kama uliweka malengo, umeyafikia kwa kiwango gani? Naam kama haujafanikiwa vizuri, basi naamni somo hili litakusaidia katika kujipanga kwa mwaka 2012 ili kama kwa neema ya Mungu tukifika Desemba 2012 unapofanya tathmini ya mwisho wa mwaka uwe na sababu ya kumshukuru Mungu kwa namna alivyokusaidia kuyafikia malengo yako.
Nawatakia sikukuu njema ya xmas na mwaka mpya
Imetolewa leo 14122011 na
Japhet mukala
Mwenyekiti-chama cha vijana wa kanyigo waishio Dar es salaam

Monday, December 12, 2011

UTARATIBU WA KUTOA HOJA BINAFSI

Kutokana na ukweli halisi wa chama chetu kufuata misingi ya haki na usawa kwa wanachama wetu, uongozi unatoa nafasi kwa mwanachama yeyeto yule ambaye amehudumia chama kwa zaidi ya miezi sita (Probation period) , kutoa dukuduku lake kwa njia yoyote iwe moja kwa moja kwa uongozi au kwa njia ya barua, na kama ilivyo ada, kila mwisho wa vikao vyetu vya jumapili ya mwanzo wa mwezi huwa tunatoa muda wa maswali na majibu kuhusu jambo lolote linalohusu chama, lengo la nafasi hii ni kutoa ushiriki mpana kwa mjumbe kuondoa dukuduku lolote juu ya jambo amabalo analiona sio sawa au anaweza kuwa anataka ufafanuzi au anashauri au anataka maelezo toka kwa mjumbe mwenzake au kwa uongozi, na kama mjumbe amadhamilia kutoa hoja nzito yenye maslahi kwa chama, anashauriwa awasiliane na uongozi mapema iwezekanavyo ili uongozi upate nafasi ya kuipitia hoja yake na kuangalia uwezekano wa kuipatia muda kwenye ajenda za mkutano unaofata, lakini pili kuona kama hoja mezani ina usahihi na uhalali wa kujadiliwa kwa maslahi ya chama.

tunaomba sana ushiriki wenu na mawazo yenu ili kuboresha chama na kutimiza malengo yetu kwa wakati
imetolewa na

Japhet Mukala
mwenyekiti wa chama
12122011

Thursday, December 8, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za pekee kwa mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kushuhudia nchi yetu ikiandika historia mpya ya miaka 50 tangu ipate uhuru wake mwaka 9 dec 1961 kutoka kwa mwingereza.

Hivi ni vipindi vya baraka na neema, ni fursa ya kufanya rejea ya kina na ya makusudi kabisa, kwa kuangalia kiundani historia, hali ya nchi na kulinganisha na hali halisi ya sasa, na hatima ya Tanzania tunayoitaka ni ipi. Ni wakati wa kujiuliza: tulikotoka, tulikofikia na matarajio yetu kwa siku za usoni .

Nichukue fursa hii tena niwashukuru vijana wenzangu, wanachama wenzangu, kwa ushirikiano wao mzuri waliouonyesha kwa kipindi chote hiki, ni mengi tumeyaona, ni mengi tumejifunza na ni mengi tunahitaji kujifunza ili kufikia malengo, yapo matatizo yaliyojitokeza na sababu za matatizo haya zipo nyingi na zinahitaji utatuzi wa haraka wenye utashi wa kiujumla na umoja wetu sisi kama watanzania. Ni wajibu wetu sisi kama watanzania kujiwekea mikakati inayotekelezeka ili kubaini mapungufu yaliyojitokeza katika historia yake ya miaka 50 yasijirudie tena au kuyapunguza kwa kiasi kikubwa.

Tafakari hii ni wajibu mkubwa, ili kujiwekea malengo na mikakati ya kuridhisha na ambayo kimsingi inaweza kutekelezeka, pale inapowezekana inawapasa watanzania kujirekebisha na kuanza kwa usahihi zaidi. Ni muda muafaka wa kuangalia tumejikwaa wapi, tumepatia wapi, je elimu ya nchi imekidhi viwango vipi, uchumi wetu unakua kwa kasi ipi na tanzania ipi tuitegemee kwa siku zijazo.
Huu ni muda muafaka kwetu sisi kama vijana, kuweka itikadi zetu pembeni na kutafakari kwa kina hatima ya hii nchi yetu, lazima tujiulize, je sisi kama vijana tuna agenda ipi inayotuunganisha sisi vijana wote wa tTnzania na kutufanya kuzungumza lugha moja ya vijana yenye utetezi, ushawishi, matumaini na uzalendo wa nchi yetu?
Mwisho kabisa nitoe rai kwa serikali yetu, kushughuklikia kero za msingi za wananchi katika nyanja za kielimu, kiafya, elimu jamii, kuhimiza uchapakazi, kutilia mkazo uzalendo toka ngazi ya chini hadi juu,dhana ya uwajibikaji ili kutoa mfano mzuri kwa vizazi vinavyokuwa, kuchukua hatua stahili mara moja pale inapohitajika, kuongeza mapambano dhidi ya rushwa kama adui mkubwa wa haki, kuhimiza uwekezaji wa ndani na kuwa na uzalendo wa kulinda, kuthamini na kutunza mali asili na mali watu.
Imetolewa leo na Japhet Mukala
Mwenyekiti-chama cha vijana wa kanyigo waishio Dar es salaam

Sunday, December 4, 2011

YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHETU CHA 04.12.2011

Kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza wale wote wlijitokeza kwenye kikao chetu cha kila jumapili ya mwanzo wa mwezi, kikao chetu kilifunguliwa saa 10.30 na kufungwa saa 12.36

baadhi ya mambo yaliyojiri ni pamoja na
1. Mwenyeki akisaidiana na viongozi wengine walieleza maana ya mkopo nini, faida na hasara zake na kutoa ushauri kwa wanachama pamoja na kutoa kijarida kinachoelezea maana halisi na mkakati kazi
2. Uchaguzi wa viongozi wa kamati za kudumu za chama ikiwa ni pamoja na  kamati ya nidhamu na uongozi, kamati ya miradi, kamati ya matukio na kamati ya fedha na  uchumi.
3. Utekeleza wa mapendekezo ya mwenyekiti wa kutafuta walezi wa chama ambapo tulikubaliana chama kiwena walezi na barua pamoja na katiba vilitumwa jana kwa wajumbe waliopendekezwa na wanachama
4.Ulitolewa ufafanuzi juu ya maana ya udhamini iwapo mwanachama ataamua kumdhamini mwanachama mwenzake.
5.Mapendekezo yalitolewa juu ya kusitisha mkopo na kutoa muda kwa wahusika kujiandaa na kuja na mikakati mizuri ya jinsi ya kuendelea na huduma hii kwa wanachama bila kuathiri maana na dhana nzima ya utoaji wa mkopo.
6.Pendekezo la kuwa na get together event kati ya xmas au mwaka mpya ambalo limepokelewa na kupelekwa kwa kamti husika yaani kamati ya matukio na tutapata taarifa yao kwa njia ya msg, face book au blog yetu kadri siku zinavyokwenda.
7.Kuanzisha mpesa na tigopesa kwa ajili ya dharura kwa wanachama ambao wapo mbali na Dar es slaam kwa kipindi cha uhitaji wa kutoa mchango wa chama au kitu chochote kinapotokea na hizi line zitakuwa chini ya wawekahazina wetu wawili ya Anderson Rwebangira na Julius Ishengoma.
8.Ilikubaliwa kuwa kila mwezi lazima watunza hazina watoe ripoti za kiutendaji, ripoti za mapato na matumizi, ripoto ya mikopo na zingine.
9. Mwisho yalitolewa mapendekezo kwamba kikao kijacho yani tarehe 08012012, hoja zote tulizoshindwa kuzimalizia kutokana na muda ndo hoja tukazo fungua nazo kikao kinachofuata pamoja na uongozi kutoa malengo ya mwaka 2012.

mwisho niwashukuru tena na kama kuna mambo ambayo wadau mngependa kupata ufafanuzi au mna mapendekezo tunawaomba kuwasiliana na uongozi wetu yani mwenyeketi na katibu kwa namba zifuatazo
Japhet Mukala-0713 362898
Denis Rutaihilwa-0716 353 466
Derick Izoba-0713 862562
Adelina Kasinda -0716 600 288
Anderson Rwebangila -0717 646 268
Julius Ishengoma -0782 429 183

Vilevile tukaribisha maoni yenu kupitia ukurasa wetu wa facebook ambao ni vijana kanyigo

imetolewa na japhet Mukala
Mwenyekiti wa chama
05122011

Thursday, December 1, 2011

MAWASILIANO YETU

Japhet Mukala-Mwenyekiti wa chama   0713 362 898
Denice Rutahilwa- Makamu M/Kiti wa chama   0716 353466
Derick Izoba - Katibu Mkuu  0713 862 562
Adelina Kasinda- Naibu Katibu Mkuu  0716 600288
Andeson Rwebangila -Muweka Hazina  0717 646268
Julius Ishengoma-Muweka Hazina Msaidizi  0782 429 183