UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Thursday, December 8, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA

Kwanza kabisa napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za pekee kwa mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kushuhudia nchi yetu ikiandika historia mpya ya miaka 50 tangu ipate uhuru wake mwaka 9 dec 1961 kutoka kwa mwingereza.

Hivi ni vipindi vya baraka na neema, ni fursa ya kufanya rejea ya kina na ya makusudi kabisa, kwa kuangalia kiundani historia, hali ya nchi na kulinganisha na hali halisi ya sasa, na hatima ya Tanzania tunayoitaka ni ipi. Ni wakati wa kujiuliza: tulikotoka, tulikofikia na matarajio yetu kwa siku za usoni .

Nichukue fursa hii tena niwashukuru vijana wenzangu, wanachama wenzangu, kwa ushirikiano wao mzuri waliouonyesha kwa kipindi chote hiki, ni mengi tumeyaona, ni mengi tumejifunza na ni mengi tunahitaji kujifunza ili kufikia malengo, yapo matatizo yaliyojitokeza na sababu za matatizo haya zipo nyingi na zinahitaji utatuzi wa haraka wenye utashi wa kiujumla na umoja wetu sisi kama watanzania. Ni wajibu wetu sisi kama watanzania kujiwekea mikakati inayotekelezeka ili kubaini mapungufu yaliyojitokeza katika historia yake ya miaka 50 yasijirudie tena au kuyapunguza kwa kiasi kikubwa.

Tafakari hii ni wajibu mkubwa, ili kujiwekea malengo na mikakati ya kuridhisha na ambayo kimsingi inaweza kutekelezeka, pale inapowezekana inawapasa watanzania kujirekebisha na kuanza kwa usahihi zaidi. Ni muda muafaka wa kuangalia tumejikwaa wapi, tumepatia wapi, je elimu ya nchi imekidhi viwango vipi, uchumi wetu unakua kwa kasi ipi na tanzania ipi tuitegemee kwa siku zijazo.
Huu ni muda muafaka kwetu sisi kama vijana, kuweka itikadi zetu pembeni na kutafakari kwa kina hatima ya hii nchi yetu, lazima tujiulize, je sisi kama vijana tuna agenda ipi inayotuunganisha sisi vijana wote wa tTnzania na kutufanya kuzungumza lugha moja ya vijana yenye utetezi, ushawishi, matumaini na uzalendo wa nchi yetu?
Mwisho kabisa nitoe rai kwa serikali yetu, kushughuklikia kero za msingi za wananchi katika nyanja za kielimu, kiafya, elimu jamii, kuhimiza uchapakazi, kutilia mkazo uzalendo toka ngazi ya chini hadi juu,dhana ya uwajibikaji ili kutoa mfano mzuri kwa vizazi vinavyokuwa, kuchukua hatua stahili mara moja pale inapohitajika, kuongeza mapambano dhidi ya rushwa kama adui mkubwa wa haki, kuhimiza uwekezaji wa ndani na kuwa na uzalendo wa kulinda, kuthamini na kutunza mali asili na mali watu.
Imetolewa leo na Japhet Mukala
Mwenyekiti-chama cha vijana wa kanyigo waishio Dar es salaam

No comments: