UONGOZI MPYA WA CHAMA 2016/17

Japhet Mukala -Mwenyekiti wa chama

Johanes Mujuni-Makamu mwenyekiti

Denice Kahangwa-Katibu mkuu wa chama

Nelson Ntoroma-Naibu Katibu mkuu

Elizeus Izoba-Mweka hazina wa chama

Agnetha Byashalila- Muweka hazina msaidizi

Hamidu Mabaraza-Msemaji mkuu wa chama

Wednesday, December 5, 2012

SHUKRANI ZA DHATI KWA WANACHAMA WOTE

habari zenu wanachama,

Kwanza kabisa kipekee kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa wema wake wote na uaminifu wake kwangu, kwa kuniongoza vema hadi siku ya leo.

Pili napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wanachama wenzangu kwa kuniamini na kunipa mamlaka ya kuongoza chama chetu kwa vipindi viwili mfululizo, kwangu ni heshima kubwa nimepewa na hakika sikuwaangusha, tumeanza chama tukiwa watu sita na shilingi sifuri hadi leo tuko wanachama zaidi ya hamsini, ni mafanikio makubwa sana na hili ni jambo la kushukuru,

Vile vile nawapongeza sana kwa uvumilivu wenu mlioonesha kwa kipindi hiki chote kwani mmekuwa pamoja nasi, tulikinzana sana kwa hoja nyingi lakini demokrasia siku zote ilitumika na maamuzi mengi yalitolewa kwa mujibu wa katiba inavyotuagiza tufanye, hili liko wazi na wanachama nyie ndo mashahidi wa hili, nimeisimamia katiba kikamilifu, tumetengeneza misingi mizuri ya chama, tumekuwa na ushirikiano wa karibu sana, umoja umejengeka, matukio mengi yaliyotokea katika kipindi chote hiki tumeweza kuyakabili kwa umoja wetu na mshikamano, na hii ndo alama sahihi ya ushiriki wenu mzuri katika uwezeshaji wa mipango ya chama kutimia kwa mujibu wa mipango sera na taratibu za chama tulizojiwekea.

Umoja wenye watu wengi kiasi hiki, lazima una mambo mengi sana yenye kukinzana sana lakini ni lazima tutumie vifungu vya sheria zetu ndogondogo tukitanguliwa na katiba, huku busara ikitawala katika kufanya maamuzi, tumelifanya hili bila kutetereka, na kwa manufaa ya chama chetu, nawashukuru sana,

Lakini ni lazima tutambue kuwa, tunayo safari ndefu sana, tulipofika sio pabaya, ni wakati sasa wa kuendeleza nguvu yetu ya ujana, akili zetu na nia yetu kuleta mawazo na fikira zenye upeo wa kujenga na kuimarisha umoja wetu ili malengo ya muda mrefu na mfupi yatimie, Kiongozi sio cheo ni kuonesha njia, hivo anahitaji sana uwepo wenu na michnago yenu ili afanye majukumu yake kwa ufasaha, tumewachagua viongozi wetu wapya sita pamoja na kamati ndogondogo kwa mujibu wa katiba, ninachoomba, juhudi mlizionesha na uungaji mkono wa yale yote tuliyofanya, naomba sana nguvu zetu tuzielekezee kwa UONGOZI MPYA, ninayo imani na hakika watu tuliowachagua hawatatuangusha, tunahitaji sana kuvumiliana, tunahitaji sana kuendeleza misingi ya kuheshimiana na kijaliana, naamini Mungu yu pamoja nasi.

Asanteni sana
Japhet
 

Wednesday, October 10, 2012

MKUTANO MKUU WA CHAMA ULIOFANYIKA 07102012

Habari zenu wapendwa,

Kwa niaba ya chama napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanachama wote waliojitokeza katika mkutano wetu mkuu wachama, tulijadili mengi sana na siku hiyo agenda kuu zilikuwa
1.Ripoti ya mweka hazina
2.Ripoti ya utendaji iliyowasilishwa na mwenyekiti wa chama aliyemaliza mda wake
3.Mabadiliko ya katiba
4.Mwenendo wa chama kwa ujumla

Niwashukuru sana kwa michango yenu ya kimawazo katika ajenda zilizoletwa, ni dhahiri kuwa zipo ajenda ambazo tulishindwa kuzijadili kutokana na muda kuwa mchache na zingine tulizijadili na makubaliano yalifikiwa, taarifa ya mwenyekiti ya utendaji na ya mweka hazina, zote zilitoa mapendekezo ambayo yote kwa pamoja hatukuyajadili kwa mapana yake ingawa tutayatengea muda wa kuyajadili na kufikia makubaliano.

Mwenyekiti wa chama alivunja rasimi uongozi uliokuwepo kwa mujibu wa katiba na kuitisha uongozi mpya ambao kimsingi utafanyika kwa mujibu wa katiba mwezi ujao ukisimamiwa na kamati maalum iliyocteuliwa kufanya mchakato mzima wa uchaguzi.

Suala la msingi ni kuomba wale wote wanaodhani wanawiwa kukitumikia chama wanaombwa kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani nafasi zote sita zipo wazi kwa sasa. uongozi ni dhamana na si cheo. tujitoa na kuonesha uzalendo kwa kusaidiana katika mchakato mzima wa kupata viongozi wanaofaa kwani uongozi ndo injini ya chama.

Tuna imani hili litafanyika kwa ufasaha na chama kitapata viongozi wake ambao watakuwa dira ya chama katika kukamilisha malengo yetu tuliyojiwekea.

Nawashukuru sana
na Mungu wabariki

Imetolewa na
Japhet Mukala

Friday, August 31, 2012

YAH MKUTANO WA CHAMA TAREHE 02092012

Ndugu mwanachama,

rejea kichwa cha habari hapo juu, unapendwa kukumbushwa kuwa siku ya jumapili tutakuwa na mkutano wetu wa kila jumapili ya mwanzo wa mwezi,

Ikumbukwe, kwa kuwa tunakaribia kufunga mwaka kichama, yapo mambo kadha wa kadha ambayo yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa viongozi, taarifa za wenyeviti wa kanda zetu kichama na kujadili umuhim wa kujadili mchakato mzima wa kupata walezi wa chama.n vilevile tutadodosa juu ya mkutano mkuu wa chama unaotazamiwa kufanyika mwezi wa kumi.

Natumaini mawazo yenu yatakuwa chachu na nguzo muhim katika kikao chetu!

Imetolewa leo na Japhet Mukala
Mwenyekiti wa chama

YAH KUSIMAMISHA UANACHAMA

Ndugu wadau,

Kwa niaba ya chama cha vijana wa kanyigo waishio Dar es salaam, napenda kuutangazia uma kuwa chama kimefuta uanachama wa Amos Mpembwe na Pendo Benard, hivyo basi naomba uma utambue kuwa hawa si sehemu ya chama kuanzia 06.08.2012.

Imetolewa na
Japhet Mukala
mwenyekiti wa chama

Monday, July 16, 2012

SHUKRANI ZA KIPEKEE KWA KUFANIKISHA SAFARI YA KUWAONA WATOTO YATIMA.


Poleni na majukumu wadau,

Napenda kuchukua fursa hii, kutoa shukrani zangu za dhati kutoka moyoni kwa wale wote waliojitokeza jana kwenda kuwaona wadogo zetu, vilevile nawashukuru wadau wengine ambao wameshiriki nasi kwa njia ya michango pamoja na kuwa mbali na Dar es salaam, vilevile sitawasahau wale wote walioshindwa kufika ila wametuma uwakilishi wao kwa namna nyingine,

Ni jambo la kumpendeza Mungu sana kw...a tukio la jana, nimshukuru Mungu sana na aendelee kututia moyo katika kuyafanya haya kwani hakuna wa kumwachia zaidi yetu sisi na wewe pia.

Naushukuru sana uongozi wa kutuo kwa ukarimu wao kwetu na niwashukuru wadogo zetu pia kwa jinsi walivyokuwa wakarimu sana kwetu,ni kweli bado jitihada za hali na mali zinahitajika sana katika kuyakamilisha haya!hakika tutafika.

Niwatakie kazi njema na Mungu awabariki pale mlipotoa awaongezee

TAFAKARI YA JUMATATU

Ukombozi wa elimu, ukombozi katika huduma za kiafya,ukombozi wa fikra, ukombozi wa utu, kamwe hautokani na pesa au uwezo fulani ulio nao, unatokana na moyo wa mtu aliona nao juu ya jambo husika!unaweza kumtegemea mbunge au diwani au waziri lakini kama hana moyo wa kusaidia hawezi kusaidia, tuchague watu wa utumishi wao uliotukuka katika mioyo ya watu na si kwa fedha na mali walizonazo!

Japhet Mukala Senior

Friday, July 13, 2012

TAARIFA KWA WANACHAMA WOTE

Kwanza kabisa napenda kuwasalimia

Nichukue fursa hii kuwapa pole na majumu yenu ya kila siku ya ujenzi wa Taifa na chama kwa ujumla, chama hadi sasa kinaendelea vizuri na tunamshukuru Mungu.

Rejea kikao chetu cha mwezi huu, nawashukuru sana wanachama wote waliojitokeza hata ambao hawakufanya hivyo lakini walitutaarifa juu ya kutoudhuria kwao, kikao kilianza mapema saa kumi na nusu na mambo mengi sana yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na Taarifa ya utendaji ya miezi sita iliyopita kutolewa na mwenyekiti wa Chama. baadhi ya mambo yafuatayo yalijadiliwa

1.Maudhurio ya wanachama hayaridhishi na hili tutalitolea ufumbuzi kwa kikao kijacho
2. Tulijadili juu ya watu wote ambao wanadaiwa na chama na barua juu ya madai zilitumwa kwa kila mwnachama anayedaiwa kuanzia shillingi moja na kuendelea
3.Tulikubaliana kuchukua maamuzi mazito ambayo tutayafanya kutokana na majibu ya barua tulizotuma kwa wanachama wenye matatizo mbalimbali kichama, na hayo maamuzi ya kamati kuu yatabarikiwa na wanachama kwenye mkutano wa mwezi wa nane.
4.Tulikubaliana pia kuwa siku ya jumapili yanai 15.07.2012 tutaenda kuwatembelea watoto yatima, nawashukuru wale wote waliojitolea kwa moyo kwa ahadi zao za mali na pesa
5.Tulikubaliana moja ya agenda za kikao kijacho ni kujadili juu ya kutafuta walezi wa chama kwani wale wote tulio walenga imeonekana wamezidiwa na majukumu

.haya ni baadhi tu ya yale tuliyoyajadili.
kwa taarifa zaidi itatolewa na katibu mkuu wa chama
Japhet Mukala

Sunday, June 3, 2012

MATUKIO YALIYOJIRI KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA ULIOPITA HADI LEO 03062012

Ndugu wanachama,

kwanza kabisa nawasalimu, ninayo imani kuwa mu wazima na mnaendelea vizuri na shughuli zenu za ujenzi wa taifa na chama chetu kwa ujumla,

Pili ningependa kutoa taarifa fupi juu ya matukio yaliyojiri kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita kama ifatavyo

1.Tukio la kwanza lilikuwa ni kwenda kumpa pole dada Jacqueline Kahembe aliyepata ajali, niwashukuru sana wale wote waliojitokeza kwa moyo wenu mliounesha, ni kweli Jacque kaumia sana na anahitaji sara, Mungu amatangulie katika kipindi hiki kigumu sana kwake na sisi kama vijana tupo nyuma yake.

2. Tukio la pili lilikuwa kwenda kumsalimia ndg yetu Stanley Pesha, aliyefiwa na mama yake mzazi, vilevile  nichukue fura hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa moyo mliounesha, huo ndo utu na maana halisi ya jumuiya kama hii tuliyonayo! hikika ni jambo jema na la kupendeza sana. ninachowaomba, ni kuendelea kumtia moyo kaka yetu katika kipindi hiki kigumu sana kwa kuondokewa mtu muhimu sana katika maisha yetu ya hapa duniani.

3.Tukifanya get together event, ilikuwa na shughuli nzuri na kweli ilifana sana, nawashukuru sana kwa kujitokeza na kujumuika na wanchama wengine ktk hafla hiyo iliyofanyika msasani beach club!

4. Ndugu yetu bwana Fortunatus Byashalila na mkewe walibahatika kubarikiwa mtoto wa kiume, Mungu ni mwema sana na chama kinatoa salam za pongezi kwa kupata mwanafamilia mwingine ndani ya umoja wetu, mtoto wetu kwa sasa anaumwa na amelazwa hospitali ya muhimbili na baba mzazi alinihakikishia kuwa afya yake kwa sasa ni nzuri na wanategemea kuachiwa kesho yani tarehe 05.06.2012 siku ya jumanne. Tuungane na familia ya Byashalila kumuombea mtoto wetu apone haraka.


Mwisho ni washukuru sana kwa ushirikiano ambao mmekuwa mkiutoa katika ujenzi wa chama
Imetolewa leo 04062012 na
japhet Mukala
Mwenyeki wa chama

Tuesday, May 22, 2012

SALAMU ZA PONGEZI

Natumaini mu wazima wa afya,

Kwanza nichukue fursa hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa yote anayotutendea, Mungu yu mwema siku zote na hakika anatupenda,

Pili nichukue fursa hii kutoa salam na shukrani zangu za pongezi kwa wale wote waliojitokeza ktk party yetu iliyofanyika 19052012,shukrani za Kipekee ziwaendee Joymetta na Hamza kwa jitihada zao za dhati kabisa kufanikisha jambo hilo, sherehe ilikuwa nzuri sana, ni mwanzo mzuri sana na nina uhakika suala hili limetoa uhamsho wa kipekee miongoni Mwetu!

Tuzidi kushirikiana katika kujenga chama!
Mungu awe nasi na abariki kazi ya mikono yetu!
Imetolewa na Japhet Mungu
22052012

Wednesday, May 9, 2012

TAARIFA YA KIKAO CHA TANO KWA MWAKA 2012

Kwanza nichukue fursa hii kuwasabahi, pili nitoe shukrani zangu za kipekee kwa wale wote wenye nia ya dhati na walijitokeza hata wale ambao hawakujitokeza ila walitoa taarifa zao katika njia sahihi za utoaji wa taarifa,

Ni mambo meingi sana yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa kutoka kwenye kamati inayoshughulikia usajili wa chama, hatua iliyofikiwa ni nzuri, na mambo ambayo yamebaki ni barua ya utambulisho toka kwa mkuu wa wilaya, wasifu wa viongozi, pamoja na gharama zote ambazo ni takribani tzs 150,000.00.

Vilevile tulijadili umuhim wa kutilia maanani malengo makuu ya chama, chama ni cha wote hivyo kila mtu anao wajibu wa kuhakikisha tunasonga mbele na yale tunayokubaliana yanazingatiwa kwa uzito wake, hili ni jambo la muhim sana kwani ndo limetuunganisha na kuwa familia moja yenye lengo la kukuza upendo na mshikamano miongoni mwa wanachama. Kama uongozi, hili tutalisema na kulihubiri kila wakati ili kiloa mmoja wetu aelewe dhima halisi ya uwepo wetu na nini wajibu wetu pamoja na mipango yetu.

Vilevile tulijadili suala la kuharisha kwa shughuli yetu na sababu zilikuwa wazi, mawazo mengi yalitolewa baadhi wakisema tuhairishe kabisa wengine wakisema hapana, kama ilivyo ada yetu, chama kinaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia, mawazo mengi yaliamua hili lifanyike 19.05.2012 na lilikubaliwa hivyo. kwa maana hiyo basi siku hiyo 19052012 tutakuwa na event yetu kama tulivyokuwa tumeitangaza hapo mwanzo, mahali ni palepale, muda na maelezo mengine yatatolewa na viongozi husika.

Maazimio mengine yatatolewa/yameshatolewa na katibu mkuu wa chama kwa njia yetu ya kawaida!

niwapongeze sana na kuwatakia shughuli njema za ujenzi wa taifa letu!
kazi ni utu wa mwanadamu
tuuchukie unyonyaji na ufisadi bali tuhimize zaidi uwajibikaji wa kweli!
Tukifanya hivyo tutakuwa tumejitendea haki sisi wenyewe pamoja na taifa letu!

Imetolewa na Japhet Mukala
Mwenyekiti wa chama.

Wednesday, April 11, 2012

TODAY'S MESAGE-A FOOD OF SOUL

 Efforts and courage are not enough without purpose and direction,
ahead on this Do not let the hero in your soul perish to fulfil the said,
Check your road and the nature of your battle n believe that you are a
high achiever. The world you desired can be won. It exists, it is real,
it is possible, it is yours

with regards
japhet

Tuesday, April 3, 2012

TAARIFA YA KIKAO CHETU CHA CHAMA KILICHOFANYIKA 001.04.2012

Habari zenu wanachama,

Nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za pekee kwa wanachama wote kwa moyo wenu na suhirikiano mnaoendelea kutupa katika kusukuma gurudumu hili lililo mbele yetu, ni kazi kubwa inayohitaji moyo lakini inatupa hamasa sisi kama viongozi kwa sababu moja tu, ushirikiano mnaotoa kwetu, ni jambo la kupendeza na kumshukuru Mungu pia.

Rejea na kichwa cha habari hapo juu, kikao chetu kilifana sana na mambo kadha wa kadha tuliyajadili na kufikia muafaka na mengine bado hatujafikia muafaka ingawa michakato bado inaendelea na tutaendelea kutoa taarifa za kiutendaji kadri tutakavyoweza na kadri mwenyezi Mungu atakavyotusaidia.

Ajenda kuu ilikuwa ni kujadili mabadiliko makubwa ya katiba na kupokea mapendekezo ya wanachama kwa njia ya mjadala kwani suala hili lilipewa muda mwingi kwa sababu ya upana wake na mwisho tulikubaliana mambo mengi ikiwa ni pamoja na

1. Uongozi utakaochaguliwa utatoa huduma kwa kipindi cha miaka miwili
2.Suala lolote la chama linalotakiwa kuamriwa kwa njia ya kura lazima liungwe mkono na theluthi mbili ya wanachama
3.Mkutano mkuu utakuwa halali iwapo utaudhuriwa na theluthi mbili ya wanachama wote
4.Sababu zitakazokubaliwa za mtu kutofika ni Ugonjwa, kuwa nje ya mji kikazi au dharura yoyote ile inayokubalika kulingana na uzito wake utakavyokuwa na taarifa zitumwe kwa katibu mapema sio chini ya masaa 6 kabla ya mkutano.


Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo kimsingi tumeafikiana ikiwa ni pamoja na kupitsisha mabadiliko makubwa ya katiba,

Vilevile suala la kusajili chama linaendelea vizuri na jambo la msingi lililotuchelewesha ni katiba, lakini kwa sasa nadiriki kusema kuwa muda si mrefu tutafikia hatua nzuri kwani katiba ilikuwa lazima ikidhi vigezo vya wizara ya mambo ya ndani.

Katiba imetamka wazi kuwa kuna mambo ambayo hayajatajwa kwenye katiba ila chama kitakuwa na sheria ndogondogo (by laws) ambazo zitasaidia kusimamia na kutoa uelekeo wa shughuli za chama.

Mwisho niwakumbushe kujitokeza kwa wingi siku ya 14.04.2012 ambapo chama tutajumuika pale msasani club na utaratibu mzima utatolewa na viongozi wa kamati husika kama tulivyokubaliana.

Nawashukuruni nyote na mungu awabariki
Imetolewa na Japhet Mukala
Mwenyekiti wa chama
03.04.2012

Wednesday, March 28, 2012

UNAKARIBISHWA KWENYE KIKAO CHA CHAMA 01.04.2012

Ndugu mwanachama,

Nipende kuchukua fursa hii, kuwakaribisha kwenye kikao chetu cha chama cha kila jumapili ya mwanzo wa mwezi, kikao kchetu kitakuwa na mambo mengi ya kujadili na zaidi kitajikita kwenye mabadiliko makubwa ya katiba ambayo yamefanywa na uongozi wa chama uliopewa na baraka na wanachama kufanya hivyo ikiwa ni katika harakati za kuafanya usajili wa chama kisheria, pili tutajadili kidogo juu ya trip yetu tunayotakiwa kuifanya 14.04.2012 kama tulivokubaliana,

Muda wa kikao ni uleule saa kumi kamili kikao kitaanza na mahali ni TP Mazembe ubungo plaza, nawakaribisha nyote, chama ni chetu kwa ajili ya maendeleo yetu.

Imetolewa na
Japhet Mukala

Monday, March 19, 2012

TAARIFA FUPI YA KIKAO CHA VIONGOZI WA CHAMA

habari za weekend wadau!

Rejea makubalianao ya kikao cha chama kilichopita, jumamosi tulifanya kikao cha viongozi wa chama, mambo mengi yalifikiwa muafaka ambayo ni pamoja na kufanya marekebisho ya katiba, ni mabadiliko makubwa sana tumeyafanya ili tuwe na katiba nzuri yenye kukidhi matakwa ya sasa na baadae ya chama, kiako kilianza sa 10.30 na kumalizika sa 12.30, maazimio ya kikao yote yataelezewa siku ya 01.04.2012 ambapo tutafanya mkutano wa chama wa mwanzo wa mwezi! nawatakia kazi njema za ujenzi wa taifa!

Imetolewa na
Japhet Mukala

Monday, March 12, 2012

SHUKRANI KWA WOTE WALIOJUMUIKA NASI KWENDA KUMPONGEZA MAULID ABDALLAH

Nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote waliojitokeza kwenda kumtembelea na kumpongeza Bwana Maulid Abdallah na famila yake kwa kupata mtoto, ni jambo jema na la kufurahisha kwa moyo mliouonesha, maudhurio yalikuwa ya kuridhisha na Maulid pamoja na familia yake wanashukuru sana kwa upendo tuliouonesha,zaidi niwatakie afya njema na tuendelee na moyo huo katika siku za usoni!

Mungu awabariki wote
Japhet Mukala
12.03.2012

Monday, March 5, 2012

TAARIFA YA MKUTANO WA CHAMA ULIOFANYIKA 04.03.2012

Kwanza kabisa nichuke nafasi hii kuwashukuru wale wote waliojitokeza kwenye mkutano wa jana na hata wale walioshindwa ila walitoa taarifa juu ya kutofika kwao!

Mkutano wetu wa jana ulikuwa na manufaa mengi sana kwani mambo muhim sana kwa uhai wa chama yalijadiliwa na kufikiwa muafaka, niwapongeze wote waliotoa michango yao kwa njia mbalimbali,

baadhi ya mambo amabayo chama kinatakiwa kuyafanyia kazi ni kama yafuatayo.;-

1.Kufanya marekebisho ya katiba ili kukidhi vigezo vya chama cha kijamii kwa mijibu wa wizara ya mambo ya ndani ikiwa ni harakati za kusajili chama chetu kitambulikane kisheria
2.Kuandaa safari yetu tuliyopanga kuifanya tarehe 14.04.2012

Haya ni mabo ambayo uongozi umepata baraka kutoka kwa waanachama kujadili na kuja na majibi kwenye kikao kinachokuja cha tarehe 01.04.2012

mwisho nitoe tena shukrani zangu za dhati kwa uongozi kwa kazi nzuri wanayoifanya kuanzia kwa katibu na msaidizi wake, muweka hazina na msaidizi wake, makamu mwenyekiti wangu na viongozi wa kamati zetu za chama, tuenedelee kuwa na umoja, nidhamu na juhudi tunayoionyesha ili hazima na malengo ya chama yatimie!

imetolewa 05032012
Na Japhet mukala
Mwkt wa chama

Monday, February 27, 2012

MKUTANO WA CHAMA 04.03.2012

Kwanza nichukue fursa hii kuwasabahi, natumai nyote mu-bukheri wa siha njema!
Ningependa kutoa wito kwa wanachama wenzagu kuhudhuria kikao chetu kama ilivyo ada ya chama kikatiba, makutano yetu ni palepale na muda wa mkutano kuanza ni saa 10-12! ili tumalize kwa wakati uliopangwa ni lazima tuanze kwa wakati uliopangwa!

Mwisho nitangulize shukrani zangu kwenu kwa ushirikiano mnaoutoa kwa dhati sana!
Akhasanteni sana
Japhet Mukala!

Monday, February 13, 2012

HONGERA SANA KAKA MAULID ABDALLAH

Kwa niaba ya chama, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza yeye na mke wake kwa kupata mtoto wa kiume jana 12.02.2012, wote wanaendelea vizuri, chama kinamtakia maisha mema, marefu na yenye baraka tele!

imetolewa na
Japhet Mukala
mwenyekiti wa chama

Tuesday, January 31, 2012

MIKUTANO YA CHAMA KIKATIBA


                 10. Chama kitakuwa kinafanya mikutano ya aina tatu (3)
                       kama ifuatavyo.

10.1.Mikutano ya kila jumapili ya mwanzo wa mwezi ambayo itakuwa imelenga zaidi kuwa na mawasiliano ya karibu kati ya mwanachama na mwanachama na kuangalia lipi lifanyike ndani ya chama ili kuleta ustawi imara na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha chama

10.2 Mikutano ya kila robo ya mwaka itakayopitia mwenendo wa chama kwa kila robo mwaka na kufanya marekebisho ipasavyo au kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kutoka kwa wanachama.

10.3. Mkutano wa dhararu ambao utawahusisha wanachama wote au kamati ya uongozi pindi itakapobidi kuwa hivo na hii itatokana na jambo ambalo litakuwa mbele yetu na kudhibitishwa na mwenyekiti wa chama.

Mahali pa kukutana ni TP MAZEMBE, iko nyuma ya ubungo plaza karibu sana na uwanja wa mpira, na muda ni saa tisa na nusu hadi kumi na mbili na nusu. mwanachama mwenye ajenda binafsi ili ijadiliwe na wanachama inatakiwa uwasilishwe kwa katibu mapema ili uongozi upate muda wa kuiangali umuhim wake na kuitolea ufafanuzi.

Mgeni aliye alikwa hatakuwa na fursa ya kujadili hoja au ajenda iliyoletwa mezani hadi pale atakaposajiliwa kama mwanachama kamili ingawa anaweza kupewa nafasi ya kushauri.

KARIBU KWENYE MKUTANO WETU 05.FEB.2012

Ndugu wanachama,

Mnakumbushwa kuudhuria mkutano wetu wa kikatiba siku ya jumapili eneo letu la kila siku pale ubungo!mada muhimu ni malengo ya mwaka huu, unaombwa kuwahi sana muda ni saa tisa jioni hadi saa kumi na mbili!kufika kwenu ndo mafanikio ya chama!
mkaribishe na mwenzako pia!

imetolewa na
Japhet Mukala

Monday, January 30, 2012

TANZIA

Kwa niaba ya chama, napenda kutoa salam za pole kwa ndugu yetu bwana Mbaraka Nyaigesha kwa kuondokewa na baba yake mkubwa, msiba umetokea jana huko mbeya ila mipango ya mazishi inafanyika ubungo kibangu! kwa wale wote watakaoweza naomba tukutane ubungo riverside saa kumi jioni ili twende kumpa pole!
kazi ya mola kamwe haina makosa, tumshukuru kwa kila jambo!
bwana ametoa na bwana ametwaa,
jina lake lihimidiwe
imetolewa na Japhet Mukala

Friday, January 20, 2012

SALAMU ZA PONGEZI

Kwa niaba ya chama cha vijana wa kanyigo waishio Dar es salaam, napenda kutoa shukrani za pongezi kwa bwana Dickson Nestory na mkewe kwa kubarikiwa mtoto wa kike leo alfajiri, afya za mama baba na mtoto zinaendelea vizuri, tunapenda kumtakia mtoto wetu maisha mema na marefu yenye baraka tele.


imetolewa na Japhet Mukala
mwenyekiti wa chama

Sunday, January 15, 2012

YALIYOJIRI KIKAO CHA 08012012

Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kuwashukuru wanachama wote waliojitokeza kwenye kikao chetu , yapo mengi yaliyojiri na zaidi tulitembelewa na mwl Boniphace Kahembe, alitoa nasaa zake na chama tulizipokea kwa mikono miwili,

Baadhi ya mambo tuliyokubaliana kwenye kikao chetu cha 08 jan 2012

1. Aprial tutakuwa na study tour ya bagamoyo na hamza pamoja na Joymetta walipewa jukum la kufanya tathmini ya safari nzima, ripoti yao itasomwa kikao kijacho cha mwezi february.
2. Wajumbe wote walishirikishwa kuchangia mawazo kwa njia ya maandishi juu ya nini kifanyike ndani ya kipindi cha 2012 na yatapitiwa na kamati ya uongozi, hivo majumuisho yote yatatolewa kikao kijacho cha mwezi february
3.Tulikubaliana kikao kijacho wanachama watapewa namba za uanachama ila kwa wale walijaza fomu zao vizuri na kuweka passpot size kama ilivyooagizwa na uongozi wa juu.
4. Juvenali alitoa ufafanuzi wa vijwanja kama alivyoagizwa na chama na wito ulitolewa kwa wanachama ambao wako tayari kununua wawasiliane nae,
5. Tulikubaliana kuwa kila mwaka tutakuwa tunafanya study tour mara mbili, mapendekezo ya lini na lini yatatolewa ufafanuzi kikao cha mwezi february.
6. Mkutano wa kimkakati wa kupanga malengo ya chama utakuwa unafanyika december kila mwaka baada ya uchaguzi wa viongozi, na hii ni kutoa fursa kwa uongozi mpya kupanga malengo yao na kutafuta njia iliyo nzuri zaidi ya kutekeleza katiba, vilevile ni kutoa muda mzuri wa chama kuanza mwaka na malengo tayari yanajulikana kwa wanachama.

imetolewa na japhet mukala